▼▼▼BOFYA HA USIKILIZE KAULI YAKE ▼▼▼
Staa wa muziki wa asili na mtunzi wa mashairi Bongo, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ akiwa kwenye jengo la Taasisi ya Freemason lililopo Posta jijini Dar.
BALAA! Staa wa muziki wa asili na mtunzi wa mashairi Bongo, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’, juzi alinaswa na makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kwenye jengo la Taasisi ya Freemason lililopo Posta jijini Dar na kuzua viulizo.
▼▼▼BOFYA HA USIKILIZE KAULI YAKE ▼▼▼
Makamanda wetu walipewa taarifa na mtu wa karibu na eneo hilo kuwa msanii huyo alionekana akirandaranda kwenye jengo hilo pasipo kujua lengo la kwenda mahali hapo ni lipi kama si mfuasi wa taasisi hiyo.“Jamani namwona Mpoto hapa getini kwenye jengo la Freemason. Ni muda yupo hapa, amevaa mkanzu mweupe. Sijui na yeye ni mfuasi wa hawa watu. Kama vipi muwahi wenyewe mjionee. Amepaki gari lake hapa,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuunyaka ubuyu huo, mapaparazi wetu walitinga eneo hilo na kumkuta Mjomba huyo akiwa amesimama nje ya gari lake aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T 371 DCE kwenye eneo la kuegeshea magari ya jengo hilo.
Baada ya muda, staa huyo alitoka aliposimama na kwenda kuingia kwenye jengo hilo huku baadhi ya wananchi wakimtupia macho ya mshangao.
▼▼▼BOFYA HA USIKILIZE KAULI YAKE ▼▼▼
“Jamani huyu Mpoto humo Freemason kumempataje! Au na yeye ni mshirika? Inawezekana hata mafanikio aliyonayo kwa sasa yanatokana na uwepo wake kwenye chama hicho,”alisikika mmoja wa watu hao.Ilibidi mapaparazi wetu wampigie simu na kumuuliza kuhusu uwepo wake kwenye jengo hilo ili kutatua kitendawili hicho ambapo alijibu:
Mpoto: (alikata simu na hakuwa hewani tena).