Staa wa Bongo Fleva ambaye jina lake limebeba uzito mkubwa Afrika, Diamond Platnumz amepata  mtoto  wa  kike  toka  kwa  mpenzi  wake  Zari  Hassani.

Mtoto huyo ameingia duniani saa 10 na dakika 40 Alfajir, Alhamis hii.

Haijaweza kufahamika kwa mara moja ni hospitali gani mtoto huyo amezaliwa kwa kile meneja alichosema ‘usalama wa mama na mtoto’ kwakuwa bado wapo hospitali.

Sura ya mama yangu inatosha kueleza ni kiasi gani najiskia ndani ya Moyo wangu, karibu kwenye ulimwengu @princess_tiffah,” ameandika Diamond kwenye picha hiyo juu aliyoiweka Instagram.

Awali Diamond alisema kuwa Zari angejifungulia Tanzania.
 
Top