0


Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amekimbizwa hospitali mchana huu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana leo mchaa akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa amweetoka bungeni na kwenda nyumbani kwakwe kwa ajili ya chakula cha mchana.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba amekimbizwa hospitali na sasa yupo chumba cha upasuaji.

Kwa Taarifa zilizotufikia hali yake ni mbaya sana baada ya mashambulio hayo ya risasiTOA MAONI YAKO

Post a Comment

WRITE YOUR COMMENTS HERE

 
Top