0

Wakati joto la kusubiri rais John Magufuli atangaze majina ya baraza lake la mawaziri likizidi kupanda, gazeti la Mwanahalisi limetoa baadhi ya majina yanayodaiwa kuvuja kutoka kwenye orodha hiyo.

Mmoja kati ya majina ambayo yamevuta usikivu wa wengi ni jina la aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, Bernard Membe ambaye alikuwa mmoja kati ya wagombea wa CCM waliokuwa wanatajwa kuwa chaguo la rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwana Halisi, majina mengine yanayotajwa ni pamoja na January Makamba,Dk. Asha Rose Migiro,Ridhiwani Kikwete,Peter Serukamba na Mwigulu Nchemba.

Jina jingine lililotajwa kwenye orodha hiyo ni jina la aliyekuwa Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT), Dk. Charles Kitima.
 
 Dk. Kitima anadaiwa kuwa mmoja kati ya watu waliomuamini sana Dk. Magufuli wakati akiwa Waziri wa Ujenzi na hata kumualika kuwa mgeni rasmi kwenye mahafari ya chuo hicho.
NB: Majina  haya  ni  kwa  mujibu  wa  gazeti  la  Mwanahalisi ambalo limedai kuyapata baada ya kuvuja. Rais Bado hajatangaza baraza lake la mawaziri

Hata hivyo,Rais Magufuli anatarajiwa kutangaza baraza lake la mawaziri muda wowote kuanzia sasa. 
 
Kwa mujibu wa katiba, rais anapaswa kutangaza baraza lake kabla ya kuanza kwa vikao vya bunge vya mwezi Januari.

Post a Comment

WRITE YOUR COMMENTS HERE

 
Top