▼▼▼TO SEE PHOTOS AND THE VIDEO, WATCH HERE, CLICK HERE DOWN▼▼▼

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kazi ya kuunganisha mabomba ya gesi kutoka Kinyelezi I kwenda katika mitambo ya Ubungo I na II, jijini Dar es Salaam imekamilika.


Aidha, kazi ya kuwasha mashine 10 za mtambo wa Ubungo I imekamilika na inategemewa tatizo la kukatika umeme litafikia tamati kuanzia leo.
                           
▼▼▼TO SEE PHOTOS AND THE VIDEO, WATCH HERE, CLICK HERE DOWN▼▼▼
“Kuanzia leo (jana) umeme umeanza kurudi kupatikana kwa uhakika katika mikoa mbalimbali pamoja na jiji la Dar es Salaam kutokana na mafundi kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwasha genereta 10 za Ubungo I, hivyo mpaka kesho (leo) uzalishaji umeme utakuwa umeongezeka,” alisema na kuongeza:


“Watanzania wategemee umeme wa uhakika baada ya kuanza kuzalisha umeme wa gesi ya Mtwara kwani kazi ya kuunganisha bomba la kusafirisha nishati hiyo imekamilika hivyo inatuhakikishia nchi kuwa na umeme wa uhakika hata kama mabwawa ya maji yanayotumiwa kuzalisha umeme yatakuwa yamekauka.”


Severin alisema gesi ya kutoka Mtwara inategemewa kuendesha mtambo wa Ubungo II wenye uwezo wa kuzalisha MW 105, mitambo ya Symbion MW 112 na Kinyerezi I, MW 150).


Alisema mtambo wa Ubungo I utaendelea kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ya Songosongo na kwamba Ubungo II ndiyo utumia gesi ya Mtwara kwa kuwa inatosha kuendesha mitambo hiyo.

Severine alisema uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi utaisaidia serikali kuokoa takribani dola za Marekani bilioni moja kwa mwaka, ambazo zilikuwa zinatumiwa kununua mafuta mazito ya kuzalisha
 
Top