▼▼▼CLICK HERE  FILL THE FORM AND WIN GALAXY S6▼▼▼

Wetu WAKATI nyumbani Bongo moto mkubwa umewashwa na mumewe aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, Josephine Mushumbusi amekuwa gumzo Marekani.

Kwa mujibu wa Mbongo aishiye nchini humo akitumia mtandao wake wa Instagram, mara baada ya Josephine kutua nchini humo akiwa na familia, baadhi ya Wabongo waishio humo walipata habari kupitia mitandao ya kijamii, wakaanza kumtafuta.
 ▼▼▼TO SEE PHOTOS AND THE VIDEO, WATCH HERE, CLICK HERE DOWN▼▼
“Jamani! Nimesikia kwamba, Dk. Slaa na mke wake wapo hapa Marekani. Sasa hamna namba zake? Maana tunataka kuwasiliana na mkewe,” alisema Mbongo huyo.
Baadhi ya wachangiaji walimuuliza kisa cha kumtafutia, alijibu: “Unajua tulisoma kwenye mitandao kuhusu madai ya Mchungaji Gwajima (wa Kanisa la Ufufuo na Uzima) kwamba, yeye (Josephine) amewahi kuanguka mapepo mara kadhaa.

“Lakini sasa hatujawahi kumsikia Josephine mwenyewe akijibu. Maana Gwajima alikuwa akimjibu Dk. Slaa, akaingiza na mambo ya mkewe. Sasa tunataka kujua mke naye anamjibu nini Gwajima?”
Habari zaidi zilidai kuwa, mke huyo amekuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali na mada kuu ni mke wa Dk. Slaa kuwa nchini humo, wengine wakitaka kujua kafuata nini.
Wengi wamehoji kama safari yake nchini humo na mumewe ni kwa sababu ya kujificha baada ya Gwajima kumwanika au kuna lingine.Hata hivyo, Mbongo mwingine alitupia kwenye mtandao wake wa Instgram akisema kuwa, ameshakutana na mke wa Dk. Slaa kwenye mgawaha mmoja akila maisha.

“Jamani, mke wa dokta nimekutana naye laivu. Anakula raha tu. Wabongo kule wao bado wanawashiana moto kwenye kampeni,” sehemu ya ujumbe huo ulisomeka hivyo.
Wakati f’lani mwanzoni mwa mwaka huu, mwanamke huyo akiwa na mume wake walikuwa nchini humo ambapo alionekana akiwa kwenye eneo la starehe akiendesha baiskeli.
Hata hivyo, wakati wa kuondoka nchini, Dk. Slaa mwenyewe alisema anakwenda Marekani kwa ajili ya mapumziko na kwamba atatumia kipindi hicho kujiendeleza katika kozi ya lugha na sheria.
 
Top