▼▼▼TO SEE PHOTOS AND THE VIDEO, WATCH HERE, CLICK HERE DOWN▼▼▼



Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye
NI Lowassa kina kona. Kuanzia kwenye mikutano ya hadhara, sherehe za harusi, msiba, usafiri wa daladala, meli na ndege, jina la Edwad Lowassa, mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), ndilo linalotawala.

▼▼▼TO SEE PHOTOS AND THE VIDEO, WATCH HERE, CLICK HERE DOWN▼▼▼
Taarifa kutoka mikoa mbalimbali nchini zinasema, tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza kupata kiwewe baada ya kuona uungwaji mkono wa Lowassa umekuwa mkubwa miongoni mwa wananchi na wanachama wa chama hicho. “…haata katika mikutano ya chama chetu (CCM), jina la Lowassa ndilo linalotawala. Viongozi na wanachama wetu, wamekuwa wakimtangaza Lowassa kuliko mgombea wetu Magufuli” (John Pombe Magufuli), ameeleza kiongozi mmoja wa chama hicho, mkoani Singida.


Katika Sherehe
MwanaHALISI Online limeelezwa kuwa katika moja ya sherehe za harusi ziliyofanyika jijini Dar es Salaam na ambayo ilihudhuriwa na watu wengo, Lowassa aligeuka gumzo.
Hii ilikuwa muda mfupi baada ya mshereheshaji kudai kuwa sherehe hiyo kwake ni “kama mafuriko.”
Source: Mwanahalisi Online
 
Top