0
DONGO! Mkali wa Bongo Fleva , Nasibu Abdul

‘ Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani
Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai
kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu
wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula
makombo , Risasi Jumamosi linakupa mchapo
kamili.
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘ Diamond ’ .
Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita
wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua
anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani
Jokate na Wema Sepetu ‘ Madam’
wanamuunga mkono Ali Kiba.
Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano
wa ‘ kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe
kutokubali , ameungana na Wema kuendesha
kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii
kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye
Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa
kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa
Diamond kimuziki .
Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘ mchezo
huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu
mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond
anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri
kuufahamu na kudai ameudharau maana
hauna jipya .
Jokate Mwegelo .
“ Hamna jipya waache waendelee kumpigia
kampeni ( Kiba) lakini mimi nafanya muziki
wangu, mashabiki wanafahamu . Kwa hao
watoto wa kike, hakuna kipya kwangu si
kimuziki hata maisha yao binafsi .
“ Wema namjua vizuri, Jokate ndiyo usiseme .
Mwache huyo Kiba aendelee kula makombo
kwa Jokate kama ameamua kipita njia
nilizopita si mbaya , inaruhusiwa, ” alisema
Diamond.
Jitihada za kumpata Jokate ili aweze
kufunguka kuwa anajisikiaje kuitwa makombo
na Diamond hazikuzaa matuda kufuatia simu
yake kuita bila kupokewa , jitihada zinaendelea .

Post a Comment

WRITE YOUR COMMENTS HERE

 
Top