0


Ni Kipi Hasa Kilichomuondoa Balozi Ombeni Sefue Ikulu? Atapangiwa Kazi Gani Nyingine?
Tumekuwa tukipaza sauti kuwa mtu anayeondolewa kwenye nafasi yake ya utumishi basi ni lazima zitolewe sababu za msingi za kuondolewa kwake! Haiwezekani katibu mkuu kiongozi anaondolewa kimyakimya tu huku tukiwa hatupewi sababu za kuondolewa kwake!

Kiongozi huyu alikuwa akitoa matamko mbalimbali huku rais Magufuli mwenyewe akituaminisha kuwa ni mtu wa viwango na anayekidhi kile anachokiita "speed yake" Leo kulikoni?

Hatupingi kuondolewa kwa watu hawa kama wamefanya makosa! Lah! Tunapinga namna wanavyoondolewa huku kukiwa na sintofahamu ya hali ya juu!

Tulishuhudia Daktari Hoseah akitenguliwa uteuzi wake kimyakimya! Pia wapo watumishi wengine wengi huku mambo lukuki yakifichwa!

Sasa leo tunaambiwa kuwa Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine? Ipi? Cheo cha katibu mkuu kiongozi ni cheo cha nne kwenye mhimili wa serikali! Atapangiwa kazi gani? Waziri mkuu? Makamu wa rais? Rais? Kutumbuliwa kwake kunaonyesha kuwa alikuwa na kasoro katika utendaji wake na si vinginevyo! Zipi?

Hali hii ya kufukuzana kimyakimya inaweza kuzua uhasama wa aina yake nchini! Kwanini mtu akifukuzwa na au kusimamishwa kazi zisitolewe sababu za msingi zilizopelekea kuondolewa? Nini tatizo? Tunajenga nini?

Angalizo kwa wana JF: Wakati Ombeni Sefue akitoa matangazo mbalimbali wengi wenu mlikuwa mkishangilia! Wengine mkadiriki kuandika kuwa Ombeni, Magufuli na Majaliwa wanatosha kuendesha nchi! Mkasema kuwa hakuna haja ya baraza la mawaziri! Leo Ombeni Sefue anatenguliwa mnashangilia kwa maandiko mbalimbali! Mmesimamia wapi? Hamuoni kasoro za wazi kwenye huu utenguaji wa watumishi (baadhi yao? ) Mimi ni miongoni mwa wale tunaoamini kuwa, kama ni kusafisha kwa kwelikweli! Hata Magufuli mwenyewe ni jipu!

Post a Comment

WRITE YOUR COMMENTS HERE

 
Top