0

Image captionRais John Magufuli ameagiza siku ya Uhuru itumiwe kufanya usafi

Raia nchini Tanzania wameungana na maafisa wa serikali kuitikia wito wa Rais John Magufuli wa kutumia Siku ya Uhuru kufanya usafi.

Mamia ya watu walirauka na kuanza kusafisha baadhi ya maeneo ambayo hujulikana sana kwa kuwa na uchafu na taka kwa wingi.

Mwandishi wa BBC Sammy Awami aliwapata wachuuzi na maafisa wa baraza la jiji Dar es Salaam asubuhi na mapema wakifanya usafi katika soko maarufu la Kariakoo.Image captionMaafisa wa serikali wanasaidiana na raia

Wengi wamefurahia agizo la Rais.
Magufuli aamua Siku ya Uhuru iwe siku ya kazi

Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pia amefika soko hilo la Kariakoo.

Rais John Magufuli naye amekuwa kwenye aneo la ufuo wa bahari karibu na ikulu akiwa amevalia glavu.

Katika eneo la Mwenge, wananchi pia wanajizatiti kufanya usafi. Mwandishi wa BBC Regina Mziwanda amewapata wananchi hawa wakiteketeza takataka baada ya kuzikusanya pamoja.Image captionWakazi wakichoma taka eneo la Mwenge

Hata katika maeneo ya kifahari, wananchi wamejitokeza kufanya usafi.

Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako

Post a Comment

WRITE YOUR COMMENTS HERE

 
Top