Waswahili wanasema kuishi kwingi ni kuona mengi.

Wataalamu wa kampuni moja ya bayotekinolojia ya San Diego (San Diego Biotechnology Company Epicyte) wamezalisha mbegu ya mahindi isiyo ya kawaida.

Mbegu hiyo wanasema itasaidia kupunguza uongezekaji wa watu duniani. Hiyo itawezekanaje? Ni kwamba mwanamume anapokula ugali wa mahindi hayo au chakula chochote kitokanacho na mahindi hayo, antibodies zisizo za kawaida zilizozoko kwenye mahindi hayo zinashambulia na kuua mbegu za kiume na hivyo kuzuia utungaji wa mimba.



Utengenezwaji wa antibody hizo unasababishwa na vinasaba vilivyopandikizwa kwenye mahindi. Kwa kufanikiwa kuwa na antibody hizo kwenye mahindi, wataalam hao wanasema wamefanikiwa kutengeneza mimea ya mahindi ambayo ni kama viwanda vidogo ambavyo vinatengeneza madawa ya uzazi wa mpango.

Taarifa hii binafsi imenistua sana kwa vile hatuna mpango mzuri wa upatikanaji wa mbegu kwa wakulima wetu. Makampuni ya nchi za nje yanafanya biashara ya mbegu kiholela tu.

Si ajabu mbegu hizi zimeshaingizwa kwa siri nchini bila sisi kujua. Yangu macho. Ni lazima tuwe na sera ya mbegu inayoeleweka.

Vinginevyo tutakula visivyoliwa.
 
Top