▼▼▼TO SEE PHOTOS AND THE VIDEO, WATCH HERE, CLICK HERE DOWN▼▼▼


Ni imani yangu kuwa kila mmoja wetu ana shauku kubwa kuona ni nani anaingia madarakani kwa awamu ya tano. Nami pia ni mmoja wenu na nakubaliana kuwa uchaguzi wa mwaka huu una changamoto kubwa kutokana na upinzani kuwa mkubwa kuliko ilivyowahi kutokea tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.
Nina machache ya kuwasihi viongozi wanaowania ngazi mbalimbali kwa nia njema tu ya kuwataka waendane na na kasi ya mabadiliko ya dunia na fikra kwa ujumla.

Kipindi nakua kwa kusikia maneno kama ” zidumu fikra za mwenyekiti” ilikuwa kawaida kabisa na ilikuwa sahihi kwa kipindi kile na kwa aina ya watu na uongozi wa enzi hizo lakini sio leo.
Tofauti ni kwamba enzi zile ilikuwa ni lazima iwe hivyo kwani tulikuwa ndio kwanza tunang’atuka mikononi mwa wakoloni na hivyo tulikuwa tukiamini aliye mbele yetu ndiye aliye sahihi.
Maisha ya uhuru yalikuwa mapya kwetu na hivyo ilipaswa tuyazoee taratibu huku mfumo wa kikoloni ukitutoka vichwani mwetu. Kwa sasa ni tofauti sana, kiongozi wa karne ya ishirini na moja anapaswa kukumbushwa yafuatayo;

▼▼▼TO SEE PHOTOS AND THE VIDEO, WATCH HERE, CLICK HERE DOWN▼▼▼


1. Uongozi ni nini?
Walio wengi hudhani kuwa uongozi ni kuongoza watu. Kwa maana ya kutoa maagizo ili yatekelezwe na wao wakisimamia tu. Kwangu mimi uongozi ni zaidi ya hapo. Uongozi ni kuwa na timu bora utakayoshirikiana nayo ili kuleta maendeleo na wewe ukiwa mstari wa mbele. Uongozi ni kuwa wa kwanza kujifunza na ukafunza na wengine kwa maneno mengine kiongozi ni mbegu inayotakiwa kuzalisha viongozi wengine.

2.Demokrasia ya kweli
Ndugu zanguni siasa za vyama vingi si uadui, si kuleta chuki miongoni mwetu bali ni kuwa na sera bora ili uchaguliwe.
Kura zisipotosha mpongeze aliyepitishwa na wananchi wengi zaidi kisha jipange upya. Lengo la kiongozi wa kweli siku zote ni kuwatumikia wananchi kwa kushirikiana na wananchi ili kuleta maendeleo. Na hilo halihitaji uwe madarakani wala kuru kuto tosha haikuzuwii wewe kutekeleza hilo.

3. Mabadiliko ya kweli
Onyesha mfano kwa vitendo juu ya zile zile sera zako kwa mahali ulipo kwa uwezo ulionao. Kumbuka si lazima utangazwe umepita ndipo ulete maendeleo. Sikusubiri nitangazwe kiongozi ili kuisadia shule ya msingi Igodivaha(mahali niliposoma).
Sikusubiri nitangazwe kiongozi ili kuleta mradi wa maji safi ya kunywa Mikocheni “A” shule ya msingi(ninapoishi), kupeleka madawati 250 shule mbali mbali za Dar es Salaam. Naamini unaweza kuleta mabadiliko bila kuwa madarakani kwani tayari una mtaji wa mawazo na rasilimali watu ambayo ni ya msingi sana.
Demokrasia ya kweli ni kukubaliana na matokeo ili kutoa muda wa kuleta maendeleo kwa pamoja ili maabadiliko ya kweli. Kama ilivyo kwa mataifa yaliyokomaa kidemokrasia.
4. Yeye ni kiongozi wa viongozi
Historia inaonyesha mfumo uongozi wa zamani ulikuwa kama utamaduni wa malezi kiafrika. Mkubwa akisema kasema na hakuna kuhoji, maana kiongozi alikuwa akionekana kama ndiye anayejua kila kitu na hivo yuko sahihi kwa kila jambo. Hali hiyo kwa sasa imebaki kwenye nyumba za ibada tu. Dunia ya leo watu wako huru, wameelimika na wanajitambua.
Kumwongoza mtu anayejitambua kunahitaji ushirikiano na majadiliano sio amri. Hivyo basi viongozi wote wa karne hii ni viongozi wa viongozi. Maana wanaongoza jamii inayojitambua. Naomba kuwakumbusha hilo. 

5. Ni dunia ya michezo na burudani
Hii sio dunia ya kumwambia mtoto soma ili uje kupata kazi nzuri, bali soma ili uje upate wepesi wa kukiongoza kipaji chako. Ni dunia inayoenda kujali ubunifu zaidi kuliko kukariri. Mwanamasumbwi Floyd Mayweather yeye ndie mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani, Alipocheza na Maidana alilipwa 29,600,000 yaani milioni ishirini na tisa na laki sita kwa kila sekunde moja.
Kama vile haitoshi Mtanzania mwenzetu Diamond yeye hutumbuiza kwa zaidi ya milioni 100 kwa onesho moja, sasa unaweza ukaona ni jinsi gani dunia ya leo ilivyobadilika na uchumi kujengwa na vipaji.
Karne hii kipaji si cha kufurahishia tu, bali ni kiwanda cha kufyatulia noti. Katika kampeni zinazoendelea tunashuhudia wasanii wakiwa mbele kutumia vipaji vyao majukaani, msiwasahau mkiwa madarakani.Kwani michezo na burudani ni chanzo muhimu cha kuimarisha uchumi wa nchi. Viongozi naomba mlitambue hili na mlipatie kipaumbele.

6.Atambue changamoto ya malezi
Tupo tulivyo kwa mchango mkubwa wa malezi yetu. Japo mkoloni wa kijerumani kaondoka ila kabaki katika vichwa vyetu na anashambulia mno familia zetu katika malezi yetu. Kwa 99% ya waTanzania wangali wanawalea watoto wao kikoloni, kibabe, kitemi tena na bakora za hali ya juu.
Watoto hawapati nafasi ya kujadili na wakubwa wala kuhoji, kwa kuogopa kipigo kama huu si ukoloni ni nini? Hali hiyo ndio huja kutusumbua ukubwani na hata kutojiamini mbele ya mkubwa wako, unafuata anachosema tu bila kuhoji wala kutathimini kwa kina, tunakuwa kama bendera ifuatayo upepo.
Tunajiona tuko huru ila tungali hatuko huru kujiamlia wala kuhoji kwa kuwa moja ya tamaduni yetu ni hiyo mkubwa akisema sikiliza tekeleza hata kama hujaelewa usiulize. Tunasisitiza demokrasia wakati kwenye kiini cha demokrasia hakuna demokrasia hakuna demokrasia.
Kiini cha demokrasia ya kweli ni kwenye malezi bora kwa wanetu. Tuwajengee uwezo wa kujiamini popote na kuwa huru kumuuliza yeyote jambo lolote kwa wakati sahihi. Dhana ya kumwona anaeuliza ni mjinga tuitokomeze inatufanya tuwe wajinga wa ukweli.

7. Tanzania ni kama mama serikali ni kama baba na kamwe sito wakana wazazi.
Kiongozi mwenye demokrasia ya kweli akumbuke kiapo hiki na akikubali kutoka moyoni.
Nimalize kwa kusema, kura yangu kwa sera bora. Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 
Top