Klabu ya Chelsea ya Uingereza ilimsajili beki wa kimataifa waSenegal aliyekuwa anaichezea klabu ya FC Nantes yaUfaransa Papy Djilobodji kwa dau la pound milioni 3, Chelseailimsajili Papy Djilobodji katika dakika za mwishoni kabla ya dirisha la usajili kufungwa, hivyo Septemba 4 ndio siku ambayo amewasili katika uwanja wa mazoezi.
Papy Djilobodji aliwasili katika uwanja wa Cobham ambao ndio unatumiwa na Chelsea kama uwanja wao wa kufanyia mazoezi na kukabidhiwa jezi ya Chelsea. Papy Djilobodji aliyesaini mkataba wa miaka minne ya kuichezea Chelsea, hayupo katika list ya wachezaji watakao cheza hatua ya makundi katika michuano ya UEFA.

Beki huyo atakuwa akivaa jezi namba 15 ila kwa sasa hatutomuona katika michuano ya Ligi ya Mabingwa kwani Chelsea haijajumuisha jina lake, hivyo atakuwa akicheza mechi za Ligi Kuu pekee.
 
Top