0

Msaidie Rais wako atawale.

Wengi waweanza kuhoji Mh. huyu aliahidi hiki na kile katika kampeni mbona bado hajatekeleza?

Kwenye vyanzo vya mapato Bandalini,kodi za wafanyabiashara wakubwa na wadogo anazikusanya ila kwenye vyanzo vingine kama kwenye migodi ya madini na viwandani amekuta ni madudu
Amekuta serikali imeingia kwenye mikataba mibovu ya kinyonyaji. Ninavyosema mikataba mibovu ni mibovu kwelikweli, mtakumbuka zile miswada iliyokuwa inapitishwa chapu chapu usiku wa manane na wabunge 33? Miswada hii imezarisha sharia mbovu kweli kweli. Mikataba hiyo mibovu inaleta madhara kwa nchi nzima navyosema nchi nina maana watu wake na siyo ardhi kwani ardhi haina uhai.

Kila Mh. Rais anavyochungulia kwenye vyanzo vya mapato makubwa kama ya kwenye migodi ya madini na gesi asilia anakuta kuna mkataba mbovu.

Afanyeje sasa?

Kwa wale wapenzi wa Simba Sports Club nitawakumbusha club chenu kilishiriki mashindano ya club bingwa Africa mwaka 1974, waliwatoa Linale ya Lethoto, wakawatoa Mufurila wanderlers ya Zambia, wakapangiwa Heaths of Oak ya Ghana. Mchezo wa kwanza walichezea Ghana pamoja na kushinda 2- 1 kulikuwa na mchezaji mmoja anaitwa Mohamed Pollo alikuwa anasumbua sana, kidogo tu kesha fika kwa Mambosasa golikipa, kidogo tu kawapita mabeki wote kafika kwa kipa Mambosasa na alikuwa anafanikiwa kuokoa hatari hizo.

Mwishowe Mambosasa akachoka akawabwatukia mabeki wake kwa nini wanamwachia winga Mohamed Pollo kila saa anasumbua? Wanafanya kazi gani? Beki wa kati merehemu Omary Cogo Mruya akamwuliza kipa Mambosasa ambaye naye ni marehemu " unaweza kudaka penati? Kipa Mambosasa akasema sawaaa kuliko mnamwachia tu Pollo anatamba.

Basi mpira uliofuata Mohamed Polo akapangua ngome kama kawaida yake kufika kwa Chogo akamkata kiroho mbaya ikawa penati, Chogo akamwambia Mambosasa haya penati hiyo. Mungu siyo Athuman penati kupigwa Mambosasa akaipangua na kwa rafu ile Mohamed Polo akawa amadhibitiwa.

Turudi kwenye mada Mh. Rais Kakuta mamikataba mabovu ya kinyonyaji kwenye vyanzo vya uhakika vya mapato hasa kwenye migodi ya madini,sasa je! aivunje ? Wanasheria mko teyari kusimama kwenye mahakama za duniani kutetea? WANASHERIA MKO TAYARI KUMSAIDIA RAIS ATAWALE?
WEEKEND NJEMA.

Post a Comment

WRITE YOUR COMMENTS HERE

 
Top