0

Babu wa LoliondoAmbilikile Mwasapila maarufu kamaBabu wa Loliondo ndio mmiliki wa hii post kwa leo, babu aliyejipatia umaarufu kwa kutoa dawa kwenye kikombe ambayo wengine walidai kupona magonjwa mbalimbali na wengine hawakupona baada ya kunywa kwenye miaka ya 2011 na 2012.
Kuanzia 2012 umaarufu wa Babu huyu aliefanya foleni ya watu kwenda kumuona kuchukua mpaka wiki tatu kutokana na wingi wa watu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania, Kenya na Zambia, ulianza kupotea na alipohojiwa na millardayo.com February 2013 alisema kuna muujiza mwingine unakuja watu wasubirie.
Kwenye Interview nyingine ya August 2015, Babu wa Loliondo ameibuka na kusema bado unakuja muujiza mkubwa zaidi ya ule wa mwanzo na huu ndio utaleta watu wengi kutoka mataifa mbalimbali lakini hawezi kusema ni kitu gani sababu hajaruhusiwa na Mungu kusema.
Anasema ‘wengine watakuja kwa kunywa dawa, wengine watakuja kwa mambo mengine tu ikiwemo kuona maajabu, mwanzoni niliwaambia watu kwamba tutapata foleni kubwa sana hapa na hawakunielewi ila sasa wananielewa nikisema, hayo maajabu mapya yatakua kwa mfumo wa dawa na miujiza mingine ambayo Mungu hajaniruhusu kuitaja
Ambilikile Mwasapila ‘Babu wa Loliondo’ anasema ukimya wake umetokana na muongozo wa Mungu, ataendelea kuwa kimya mpaka Mungu atakapoufungua muujiza mwingine wa pili aliomuonyesha kwenye maono miaka kadhaa iliyopita, anajua kuna kitu kikubwa kinakuja ila sio muda wake kukisema sasa hivi.
Ameandaa heka 16 kwa ajili ya miujiza hii mikubwa ambapo hata 2013 aliionyesha millardayo.com shamba hilo kubwa aliloliandaa ikiwemo kujenga nyumba za kupokelea watu ambapo kwenye huu muujiza mpya anasema lengo lake sio hela sana kwani hata ile 500 aliyokua akiitoza kwenye muujiza wa kwanza ilikua ni agizo la Mungu na sio yeye, kama safari hii Mungu atasema iongezeke atafanya hivyo, akisema iwe bura ni sawa vilevile’
Babu wa Loliondo ambaye ana umri wa miaka 81 sasa hivi, ni baba wa watoto wanne ambapo wa kike ni mmoja na wakiume watatu, mke wake alifariki mwaka 2009.

Post a Comment

WRITE YOUR COMMENTS HERE

 
Top