KUTAZAMA PICHA na VIDEO YAKE AKIWA MTUPU BONYEZA HAPA CHIN==
Gari aina ya Toyota Harrier likitolewa eneo la ajali.
Wananchi wakishuhudia gari hilo wakati likiondolewa eneo la ajali.
Toyota Harrier likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali hiyo. (Picha na Mzee wa Matukio Daima)
WATU wawili wamepoteza maisha katika ajali iliyotokea leo alfajiri saa 11: 30 katika eneo Mizani mkoani Iringa kwenye barabara ya Iringa – Mbeya.
Ajali hiyo imelihusisha lori lenye namba za usajili T 463 CRV lenye tela namba T 575 CFD lililogongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya Toyota Harrier yenye namba IT 997 iliyokuwa ikitokea Dar kwenda nchi za jirani.
Akiongea na tovuti hii, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea ajali hiyo na kueleza kuwa waliofariki dunia katika ajali hiyo ni waliokuwa kwendye Toyota Harrier ambao ni dereva Utilo Mwanasongole (50) mkazi wa Dar es Salaam na Yona Mwakilasa (22) mkazi wa Ilomba.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa, marehemu alikuwa anajaribu kumkwepa mwanakijiji aliyekuwa akiendesha baiskeli ndipo alipogongana uso kwa uso na lori hilo.
Majeruhi katika ajali hiyo ambao walikuwa katika lori wamepelekwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.